Bunge Laidhinisha Matumizi Ya Shilingi Trilioni 1.7

Bunge la kitaifa jana alasiri liliidhinisha matumizi ya shilingi trillion- 1.7 kutoka kwa hazina kuu ya serikali kwa ajili ya matumizi mbali mbali ya kipindi kinachomalizikia tarehe 30 mwezi Juni mwaka 2017. Ripoti hiyo inajumuisha pia utoaji wa shilingi bilioni-12.4 kutoka kwa hazina ya usawazishaji kugharamia matumizi kwenye jumla ya kaunti 14. Siku ya Jumanne wabunge wakiongozwa na kiongozi wa walio wachache Francis Nyenze waliapa kuto-idhinisha bajeti A�ya shilingi trillion- 2.3 iliyowasilishwa mbele yao na waziri wa fedha Henry Rotich mapema mwezi huu , kwani haikujumuisha fedha za hazina za ustawi wa maeneo-bunge CDF. Naibu Spika wa Bunge la kitaifa Joyce Laboso alilazimika kuahirisha mjadala huo kwa zaidi ya saa moja ili kuwapatia wabunge wasaa wa kujadili athari za kesi dhidi ya hazina ya CDF. Walikuwa wakilalama kuhusu kesi hiyo ambapo baadhi ya makundi ya kijamii yalikwenda mahakamani kutaka kuizuia hazina kuu kusambaza pesa hizo. Inaaminika kwamba hali ya wabunge kubadili msimamo wao ilishawishiwa na mkutano uliofanyika kati ya wabunge wa Jubilee na Rais Uhuru Kenyatta na pia Naibu wake William Ruto. Inaaminika kwamba A�viongozi hao wawili waliwahimiza wabunge kuidhinisha bajeti, na kuahirisha mazungumzo juu ya hazina za ustawi wa maeneo-bunge (CDF).