Bunge la Seneti Kuharakisha Kupitishwa kwa Mswada Kukabiliana na Utumizi wa Dawa Haramu Michezoni

Bunge la Seneti limeamua kuandaa kikao chake kesho asubuhi katika jitihada za kuharakisha kupitishwa kwa mswada wa kukabiliana na utumizi wa dawa haramu michezoni ambao ulipitishwa jana na bunge la taifa.

Hatua hiyo ni katika jitihada za kuepusha Kenya kupigwa marufuku katika mashindano ya kimataifa yakiwemo michezo ya mwaka huu ya Olimpiki jijini Rio, Brazil.

Akiwasilisha mswada huo kiongozi wa walio wengi katika buneg la Seneti Prof. Kithure Kindiki alisema kuwa Kenya imedhulumiwa bila sababu katika vita dhidi ya utumizi wa dawaza kusisimua misuli michezoni.

Kiongozi wa walio wachache bungeni Moses Wetanga´┐Ż´┐Żula alisema kuwa wanariadha mashuhuri humu nchini akiwemo Rita Jeptoo wameathirika kutokana na ushawishi kutoka kwa mawakala wenye nia mbaya.