Bunge la kitaifa latarajiwa kuwasaili mawaziri waliopendekezwa

Bunge la kitaifa wiki hii linatarajiwa kuanza kuwasaili waliopendekezwa kuhudumu kama mawaziri.Hayo yanajiri baada ya rais Uhuru Kenyatta kuwasilisha majina yao katika bunge hilo.Watu tisa waliopendekezwa miongoni mwao Monica Juma aliyependekezwa kuhudumu kama waziri wa mashauri ya kigeni, Farida Karoney waziri wa ardhi na Keriako Tobiko aliyependekezwa kuhudumu kama waziri wa mazingira wanatarajiwa kusailiwa mbele ya kamati ya bunge itakayoongozwa na spika Justin Muturi.Wabunge wa upinzani wamejitenga na shughuli hiyo ya kamati ya maswala ya uteuzi lakini wabunge wa Jubilee ambao ni wanachama wa kamati hiyo wamesema shughuli hiyo haitakuwa na mapendeleo.Umma una muda hadi siku ya jumatano kuwasilisha mapendekezo yao.Hata hivyo waliopendekezwa kuhudumu kama makatibu wa maswala ya usimamizi hawatasailiwa licha ya mwanaharakati A�Okiya Omtatah kuwasilisha kesi mahakamani dhidi ya kubuniwa kwa wadhifa huo.