Bunge la kitaifa latarajiwa kupigia kura pendekezo la kubadili tarehe ya uchaguzi mkuu.

 

Bunge la kitaifa wiki hii linatarajiwa kupiga kura kuhusu pendekezo la kubadili tarehe za uchaguzi mkuu. Mswada wa marekebisho ya katiba ya Kenya wa mwaka 2018 uliowasilishwa na mbunge wa Kiminini Gatimu Njoroge unataka kubadilishwa kwa tarehe ya uchaguzi mkuu kutoka jumanne ya pili ya mwezi Agosti kila baada ya miaka mitano hadi Jumatatu ya tatu ya mwezi Disemba.

Wakati uo huo raia mmoja amekwenda mahakamani  kulitaka baraza la mawaziri kupunguza idadi ya kaunti kutoka 47 hadi 18.Geoffrey Gatimu Njoroge pia anataka maeneo ya bunge yapunguzwe  hadi 246.

Aidha rufaa yake inataka kuanzishe mfumo wa uongozi wa kuwa na Waziri mkuu na manaibu wake wawili,ambao watateuliwa na rais.Pia anapendekeza rais kuwateuwa mawaziri 24 kutoka katika bunge.

Spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi alhamisi iliopita alimtaka rais  kusema ikiwa  kura ya maamuzi inaweza kuidhinishwa ikiamuliwa na  wabunge 233