Bunge La Kaunti Ya Nyeri Kuendeleza Hoja Ya Kumuondoa Gavana Gachagua Mamlakani

NYERIBUNGE
Wanachamwa bunge la kaunti ya Nyeri wameazimia kuendeleza hoja ya kutokuwa na imani na gavana wa kaunti hiyoA� Nderitu Gachagua ijumaa hii. Wakiongea katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa wakati mmoja diwani wa lokesheni yaA� Gakawa ,James Gathogo, wanachama hao wakiongozwa na kiongozi wa walio wengi katika bunge la kaunti hiyoA� Duncan Gituanja.

Walisema kuwa hawatabadilisha uamuzi huo kwa vile wana msingi wa kutosha wa kumwandoa mamlakani gavana huo. Wanachama hao wanamshtumu gavana huyo kwa uongozi wa kihimla huku wakidai kuwa alikataa kuhojiwa kuhusiana na swala la matumizi mabaya ya pesa.
Wakati huo huo, Gituanja ameishtumu tume ya maadili na kupambana na ufisadi na kudai kuwa inatumiwa na gavana huyo kuhujumu jitihada zao. Juhudi za mbunge wa KieniA� Kanini Kega za kujaribu kutatua swala hilo kupitia mazungumzo ziliambulia patupu.