Bunge la Italia lapendekeza kupeleka jeshi la wanamaji katika bahari ya Libya

Bunge la Italia linajadilia mapendekezo ya kupeleka jeshi la wanamajiA� katika eneo la bahari la Libya kuwasaidia walinzi wa pwani ya nchi hiyo kukabiliana na ulanguzi wa watu. Bunge la Lower limeunga mkono wazo hilo ambapo wabunge 328 wanaliunga mkono huku wabunge 113 wakilipinga. Baraza la mawaziri la Italia linataka jeshi lake la wanamaji lipelekwe nchini Libya kuisaidia Libya kukabiliana na ulanguzi huo wa watu. Pia Italia itaisaidia Libya kuanzisha kituo cha kuchunguza shughuli za baharini nchini Libya. Wapiganaji mashariki mwa Libya wametishia kuchukua hatua za kuizuia Italia kuingilia shughuli za nchi hiyo kiholela.