Bunge kurudia vikao vyake leo

Bunge linatarajiwa kurejea vikao vyake  hivi  leo baada ya likizo ya majuma mawili. Shughuli kuu ni kujadili  na kuidhinisha  watu walioteuliwa kuhudumu katika baraza la mawaziri. Kamati ya bunge kuhusu uteuzi itawasilisha ripoti yake baada ya kuwasaili  watu tisa walioteuiliwa kuhudumu katika baraza la mawaziri Alhamisi na Ijumaa iliyopita.   Walioteuliwa  ni:  John Munyes wa wizara ya Mafuta ya Petroli na Madini, Monica Juma wa Mashauri ya Kigeni,  Farida Karoney  wa ardhi na Nyumba,  Peter Munya wa Maswala ya Afrika Mashariki na Ustawi wa  Miradi ya miundo msingi kueleklea kaskazini mwa nchini na  Profesa Margaret Kobia wa Utumishi wa Umma, Vijana na Jinsia. Wengine walioteuliwa ni:  Keriako Tobiko wa Mazingira na Misitu,  Simon Chelugui wa Maji na Usafi, Ukur Yatani wa Leba na Huduma za Jamii  na   Rashid Achesa  wa Michezo na Turathi. Wabunge hao kadhalika watateuwa wanachama wa Tume  ya Kuajiri Wafanyakazi wa Bunge baada ya  waunge wa chama cha Jubilee na muungano wa NASA kutofautina kuhusu orodha ya awali iliyowasilishwa mwaka uliopita ili iidhinishe.  Wakati huo huo, bunge la seneti linatarajiwa  kuidhinisha  wanachama wa kamati ya shughuli zake.