Bunge kurejelea vikao Alhamisi

Spika wa bunge la taifa Justin Muturi na mwenzake wa Senate Ekwee Ethuro wameidhinishwa kuwania tena nyadhifa zao wakati bunge litakaporejelea vikao vyake siku ya Alhamisi. Muturi atawania wadhifa huo na wawaniaji wengine wawili, Noah Migudo na Washington Odhiambo. Hata hivyo ni kinyanga��anyiro cha spika wa bunge la Senate ambacho kimewavutia watu kadhaa huku Ethuro akitarajiwa kuwa na upinzani mkali kutoka kwa wawaniaji wengine miongoni mwao aliyekuwa gavana wa Bungoma Ken Lusaka. Wengine ni aliyekuwa naibu wa spika wa bunge la taifa farah Maalim, aliyekuwa Seneta wa Migori Wilfred Machage, James Gesami, Paul Ribathi na Ramesshchandra Govind. Kuchaguliwa kwa Mbunge wa Kuresoi Kaskazini Moses Cheboi kuwa naibu wa spika wa bunge la taifa kunatarajiwa kuwa shwari kwani ni yeye pekee ambaye ameidhinishwa na katibu wa bunge kuwania wadhifa huo. Seneta wa kaunti ya Muranga��a Irungu Kanga��ata, Seneta wa nairobi Johnson Sakaja, seneta wa Kiambu Kimani Wamatangi na seneta wa Nakuru Susan Kihika watawania wadhifa wa naibu wa spika wa bunge la Senate. Haya yanajiri huku kukiwa na tisho kutoka kwa muungano wa NASA la kususia hafla ya kuapishwa kwa wabunge. Muungano wa NASA unataka bunge la 12 kuapishwa mararufaa kuhusu uchaguzi wa urais itakaposikizwa na kuamuliwa.