Bristol City kuchuana na Manchester City kwenye nusu fainali

Timu inayoshiriki ligi ya daraja ya pili Bristol City itachuana na Manchester City katika nusu fainali ya kombe la Carabao, nayo Chelsea imenyane na Arsenal katika nusu fainali ya pili.Manchester City na Chelsea zitakuwa nyumbani katika mechi za mkondo wa kwanza, juma la tarehe nane mwezi January, huku mechi za mkondo wa pili zikichezwa majuma mawili baadaye. Bristol City iliwashinda mabingwa watetezi Manchester United mabao 2-1 jana usiku na kufuzu kwa nusu fainali. Manchester City iliibandua Leicester kwa njia ya penalty, Chelsea ikailemea Bournemouth mabao 2-1 nayo Arsenal ikaishinda West Ham bao moja kwa bila.