Bonnie Musambi

Bonnie Musambi ni Mtangazaji wetu wa kipindi cha asubuhi maarufu ‘Zinga la Asubuhi’ kuanzia saa kumi na mbili hadi saa nne kila Jumatatu hadi Ijumaa. Kwenye kipindi hiki ambacho amekifanya tangu mwaka 2008, Bonnie amebandikwa majina ya kistadi na mashabiki wake. Majina haya ni pamoja na: Le giant de la press africain, Kijana Mtall na Bonnie Bonnie.

Mbali na kuwa msomaji habari za Kiswahili kwenye runinga yetu KBC Channel One, Bonnie huendesha mahojiano kwenye kipindi cha BBC Sema Kenya. Aidha ni msanii wa nyimbo za injili na jina lake katika sanaa ni GAFA B pia ni mzungumzaji lugha ya Lingala, M.C, ameoa na ana mtoto mmoja. Kwa sasa anaendeleza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Daystar.

Mfuate kwenye mtandao wa Twitter @bonniemusambi au Facebook Bonnie Musambi a.k.a Bonnie Bonnie

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *