Boinnet ahakikishia wakenya uchaguzi wa amani

Inspekta jenerali wa polisi Joseph BoinnetA�amesema huduma ya polisi itahakikisha kuwa uchaguzi mkuu wa tarehe 8 mwezi ujao unaandaliwa kwa njia ya amani kwa heshima ya marehemu waziri wa usalama wa taifa Joseph Nkaissery. Boinnet amesema walikuwa na ushirikiano mwema kikazi na marehemu Nkaissery na kwamba huduma hiyo itakosa ushauri wake. Boinet amesema hayo huku mkewe marehemu Hellen Nkaiserry akitoa wito kwa Wakenya kukoma kueneza uvumi kuhusiana na kifo cha mumewe na kukubali matokeo ya uchunguzi wa watalaamu.Alisema marehemu mumewe alikuwa mtu mnyenyekevu na mwenye bidii,ambaye wakati wote alikuwa tayari kusaidia .Alisema hayo wakati wafanyakazi kutoka wizara ya usalama wa taifa walipomtembelea nyumbani kwake Karen leo asubuhi.Ibada ya wafu ya marehemu itaandaliwa kesho katika kanisa la BaptistA� la Ngong Road saa nane alasiri na atazikwa siku ya Jumamosi nyumbani kwake katika eneo la Ilbisil kaunti ya Kajiado. Marehemu alifariki siku ya jumamosi iliyopita kutokana na mshtuko wa moyo.