Wanafunzi wa vyuo vikuu vya kigeni wanufaika na utoaji mikopo ya elimu

RaisA� Uhuru Kenyatta amesema wakenya wanaosomea vyuo vikuu vya kigeni wanafaa kunufaika na pesa za bodi ya utoaji mikopo ya elimu ya juu. Rais amesema kulingana na sera ya serikali kila mwanafunzi mkenya anayesomea chuo kikuu kinachotambulika anahitimu kupatiwa mikopo ya bodi hiyo na ndiyo sababu wale wanaosomea vyuo vikuu vya kibinafsi wanapatiwa mikopo hiyo.

Rais aliyasema haya alipokutana na zaidi ya wanafunziA� 500 wa Kenya mjiniA� Khartoum, ambao ni miongoni mwa wakenya wapataoA� 800 ambao aliwahutubia katika siku ya pili ya ziara yake rasmi nchini Sudan.Wakenya hao pia walijumuisha walimu wanaofundisha katika shule za kifahari nchini Sudan. Rais Kenyatta aliwahimiza wanafunzi wakenya kujisajili zaidi kwa masomo katika sekta ya mafuta na uchimbaji madini .

Rais aliwaambia wanafunzi hao kuwa ameomba serikali ya Sudan kuwapa uanagenzi wanafunzi wakenya wanaosomea masomo ya kiufundi. AlisemaA� Sudan imepiga hatua kubwa katika sekta zaA� petroleum na gesi na uchimbaji madini licha ya kukumbwa na vikwazo kwa miaka mingi. Mkutano huo ulihutubiwa na na balozi wa Kenya nchiniA� Sudan, Aron Suge.