Bodi ya ukaguzi wa filamu kuangazia vivutio vya watalii katika eneo la pwani

Bodi ya ukaguzi wa filamu nchini itashirikiana na watayarishaji filamu wa hapa nchini katika kuangazia vivutio vya watalii katika eneo la pwani.haya ni kwa mujibu wa maneja wa eneo la pwani wa bodi hiyo,Bonventure Kioko.Akiongea na wanahabari,afisa huyo alisema ipo haja ya kuonyesha vivutio vya watalii,utamaduni na maanthari ya Kenya kwenye filamu zinazotayarishiwa hapa nchini.Alisema ni muhimu kuangazia utamaduni wa Kenya na turathi zake kwenye filamu.Kioko alisifu tamasha ya kila mwaka ya utamaduni wa Lamu ambayo alisema imechangia pakubwa katika kuimarisha utalii katika eneo la pwani.A�