Bingwa wa mbio za mita elfu tano,Hellen Obiri ana imani ya kuendeleza msururu wa ushindi wake

Bingwa wa mbio za mita elfu tano duniani, Hellen Obiri, ana imani kuendeleza msururu wake wa ushindi katika mbio hizo.

Wakati wa michezo ya mwaka 2014, Obiri alishiriki katika mbio za mita 1500 na kumaliza katika nafasi ya sita. Wakati huu anajiandaa kushiriki kwenye mbio za mita elfu tano nchini Australia, na anaamini atanyakua nishani ya Dhahabu jinsi alivyofanya mwaka 2017, katika mashindano ya riadha ya dunia, jijini London.A�Wakati wa michezo ya mwaka 2014, Kenya ilimaliza katika nafasi ya kwanza katika riadha baada ya kutwaaA�A�nishani kumi za Dhahabu, kumi za Fedha na tano za Shaba.