Binadamu mnyama

Msichana wa miaka minane amepatikana akiishi na tumbili katika hifadhi moja ya wanyama pori huko Bahraich, Kaskazini mwa India.Msichana huyo ambaye alipatwa na afisa wa polisi aliyekuwa akishika doria alikuwa akitembea kwa miguu na mikono na hana uwezo wa kuzungumza. Maafisa wamesema msichana huyo haoniA� tatizo kuishi na wanyama hao katika hifadhi hiyo lakini wameongeza kuwa wangali wakijaribu kubainisha msichana huyo ni nani ,alitoka wapi na ameishi katika hifadhi hiyo ya wanyama kwa muda gani. Ingawa amefundishwa kutembea kwa miguu ,msichana huyo anakula na kutembea kama mnyama na hutoroka anapoona binadamu.