Bikizee Wa Miaka 84 Akamatwa Kwa Kucheza Kamari

Polisi nchini Thailand wamemkamata bi kizee mwenye umri wa miaka 84 katika msako wa majumba ya kuchezea kamari mjini Pattaya.

Raia 32 wa kigeni walinaswa katika operesheni hiyo fumanizi.

Utawala wa kijeshi nchini humo unajitahidi kupigana na kuenea sana kwa mchezo wa kamari ambao unaambatana na uvunjaji wa sheria.

Rais hao walipatikana na kadi nyingi kupita kiasi ambazo hazijasajiliwa rasmi na afisi inayosimamia kamari nchini humo.

Kati ya wageni 32 waliokamatwa 12 walikuwa waingereza 3 Norway,3 Sweden, 2 Australian , Mjerumani mmoja na raia mmoja kutoka Denmark, Canada na New Zealander.

Jumba hilo la kamari ya chini kwa chini liligundulika baada ya mtu mmoja kupasha habari tume ya kupamabana na ufisadi kuhusu kuwepo kwake.

Wanakabiliwa na makosa ya kuvunja sheria ya mwaka wa 1935 ya kumiliki zaidi ya kadi 120 kinyume cha sheria.

Thailand inasheria kali sana dhidi ya uchezaji kamari wa aina na hali yeyote.

 

Kutoka BBC