Biashara ya hoteli kuimarika jijini Mombasa kufuatia ongezeko la watalii

Wenye hoteli jijini Mombasa na viungani mwake wameripoti kwamba biashara zao zimeimarika kufuatia ongezeko la watalii wa humu nchini na wale wa kigeni. Wanasema kuwa ongezeko la watalii wa humu nchini limetokana na nauli nafuu kufuatia kuzinduliwa kwa huduma za treni za Madaraka express. Hoteli nyingi pia zimebuni huduma maalum kwa familia mbali mbali ili kuvutia wageni zaidi. Wakati huo huo, ukosefu wa mbinu bora za kutambua mifugo katika jamii za wafugaji wa kuhama-hama zimeathiri biashara ya mifugo katika maeneo husika. Wajumbe kwenye warsha ya siku mbili ya wabunge kutoka maeneo ya wafugaji wa kuhama-hama huko Mombasa pia walielezwa kuwa sekta ya ufugaji inapaswa kuboreshwa ili kuvutia wawekezaji. Kwingineko, wakulima wametakiwa kukausha mahindi yao barabara ili kuepuka visa vya mahindi hayo kuharibiwa na kuvu yaani-aflotoxin. Mhadhiri wa chuo kikuu cha Nairobi, Prof. Sheila Okoth amesema uhifadhi bora wa nafaka utazuia nafaka hiyo kuharibiwa na kuvu. Prof Okoth kuwe na vifaa bora vya maabara katika taasisi za elimu ya juu kwa minajili ya kutambua mapema visa vya kuvu.