Biashara nzuri msimu wa krismasi kufuatia ongezeko kwa watalii

Hoteli za ufuo wa bahari hindi jijini Mombasa na viungani mwake zimekuwa na biashara nzuri msimu huu wa krismasi kufuatia kuongezeka kwa watalii wa kutoka humu nchini ambao wamemiminika jijini humo kusherehekea krismasi katika mkahawa wa Travellers Beach Hotel wakati wa karamu ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na wasimamizi wa hoteli hiyo kwa wateja wake, maneja wa mauzo na masoko wa hoteli hiyo,Wafula Waswa alisema biashara imeimarika msimu huu wa krismasi huku mamia ya watalii wakimiminika jijini Mombasa.Wafula,alisema hoteli za north coast na south coast zimejaa watalii kufuatia kuzinduliwa kwa huduma za usafiri kwenye reli ya kisasa kati ya Nairobi na Mombasa.Terry Gore,mtalii kutoka Denmark alisema ana furahia kusherehekea krismasi ya mwaka wa 30 na mwaka mpya jijini Mombasa kwasababu ya maanthari yake. Gore alitoa wito kwa mataifa ya Ulaya kuwahimiza raia wao kuzuru kenya.