Bi. Margaret Kenyatta awarai wanawake wa jamii ya waluo kupigia kura Juilee

Mama taifa Bi. Margaret Kenyatta amewarai wanawake katika eneo la jamii ya Waluo huko Nyanza kuazimia kuchagua kuendelea kwa ufanisi hapa nchini kwa kumpigia kura rais Uhuru Kenyatta. Kwa kuunga mkono muhula wa pili wa rais Uhuru Kenyatta mamlakani, mama taifa alisema wanawake pia watakuwa wanamruhusu kuendeleza na kupanua ule mradi wake wa Beyond Zero ambao juhudi zake zimewafikia na kubadilisha maisha ya mamilioni ya wanawake kote nchini.A� Mama taifa alitoa wito kwa wanawake katika kaunti za Kisumu, Migori, Siaya na Homa-Bay kupiga kura kwa dhamira zao huku wakitilia maanani haja iliyopo ya kudumisha amani hapa nchini. Mkutano huo ulioandaliwa na shirika la Maendeleo ya Wanawake ulikuwa hafla ya kumi ya aina hiyo kufuatia mikutano sawia na hiyo huko Kitui, Kajiado, Isiolo, Samburu, Kisii, Nyamira, Kwale, Nakuru na Kakamega katika wiki za hivi majuzi. Mkutano huo pia unafikisha 35 idadiA� ya kaunti ambazo mama taifa amepeleka ujumbe wake wa kuwapa uwezo wanawake na ambako pia amepigia debe kuchaguliwa tena kwa rais Uhuru Kenyatta.