Bi. Margaret Kenyatta atoa wito wa amani kwa Wakenya

Mama wa taifa Bi. Margaret Kenyatta ametoa wito kwa Wakenya kudumisha amani wakati wa marudio ya uchaguzi wa Urais. Mama wa taifa alisema kwamba bado kutakuwa na nchi ya Kenya baada ya uchaguzi, na hivyo ni muhimu kudumisha amani. Akihutubia mkutano wa shirika la Maendeleo Ya Wanawake (MYWO) , katika kituo cha Bura, kaunti ya Taita Taveta, Mama wa taifa alihimiza pia wapigaji kura wa eneo la Pwani kumchagua Rais Uhuru Kenyatta wakati wa marudio hayo ya uchaguzi wa Urais. Alisema kwamba kura kwa Rais Kenyatta zitamwezesha yeye kuendelea na miradi yake ya kubadili maisha ya watu, kote nchini. Wakati wa ziara hiyo Mama wa taifa, alitembelea kijiji kimojaA� huko Taita Taveta, naA� kuzindua mradi wa ufugaji KukuA� utakaonufaisha zaidi ya familiaA� elfu-1 kwenye Kaunti hiyo. Bi. Kenyatta alisema mradi huo unalenga kuboresha maisha ya watu,A� hususan wanawake ambao ndio uti wa mgongo wa familia. Mradi huo ni ushirikiano kati ya ule wa ofisi ya Mama wa taifa wa (Beyond Zero) naA� a�?Ahadi Kenyaa�?.