Bernad Mang’oli kujiunga na kikosi cha Harambee Stars

Aliyekuwa nahodha wa timu ya AFC Leopards, Bernad Mang’oli amesema A�ana imani ya kujumwishwa katika kikosi cha a�?Harambee Starsa�� baada ya kuwa nje kwa muda mrefu.A�A�Mang’oli, aliyetia saini mkataba wa miaka miwili na kilabu cha Sofapaka wakati wa uhamisho, A�amesema ingawa ananuia nafasi hiyo, ataendelea kujitahidi zaidi mchezoni.A�A�Kiungo huyo hatacheza dhidi ya Zoo Kericho uwanjani Narok baada ya kuumia lakini amethibitisha kuwa anaendelea kupata nafuu. Wakati uo huo,A�Hillary Echesa anaamini Sofapaka itaishinda timu ya Zoo Kericho, timu hizo zitakapochuana kesho. Echesa anaamini kuwa mchezo ulioshuhudiwa dhidi ya Tusker uliwapa Sofapaka, matumaini ya kufanya vyema kesho.