Benki Ya KCB Yanakili Nyongeza Kubwa Ya Faida

Benki ya Kenya Commercial imenakili nyongeza ya faida ya asilimia 16 baada ya kulipa ushuru kufikia shilingi bilioni 19.6. Faida hiyo, banki yenyewe ilisema yatokana na ongezeko la mapato ya kutokana na riba na kuboreka kwa utendakazi wake. Benki hiyo imeongeza kuwa hali hiyo imetokana na juhudi zake za kujiimarisha kibiashara licha ya hali ngumu ya kiuchumi katika kanda ya Afrika Mashariki. Benki hiyo imependekeza mgao wa faida wa shilingi mbili kwa kila hisa. Katika muda wa mwaka mmoja uliopita benki ya KCB imeweza kujiimarisha katika utoaji mikopo kupitia ushirikiano na ubunifu na kampuni ya Safaricom. Mwaka uliopita benki hiyo ilitoa mikopo ya zaidi ya shilingi bilioni 7 kwa zaidi ya wateja milioni 5 wa huduma ya KCB-Mpesa. Hali hiyo iliwezesha kiwango cha mikopo ya benki hiyo kuongezeka kwa asilimia 22 kufikia shilingi bilioni 346. Benki ya KBC inanuia kupanua huduma zake hadi nchiniA�Ethiopia, Somalia, Msumbiji na Jamhuri ya Demokrasia yaA� Congo .