Benki ya Gulf Africa Yaunga Mkono Mswada wa Kudhibiti Viwango Vya Riba za Mikopo

GULF BANK
Benki ya Gulf Africa imeunga mkono mswada wa kudhibiti viwango vya riba za mikopo uliopitishwa na bunge la kitaifa. Mkurugenzi mkuu wa benki hiyo, Abdalla Abdukhalik tayari amewasilisha memorandum kwa benki kuu ya Kenya na anashauriana na wadau wengine kuhusu jinsi ya kudhibiti viwango hivyo vya riba za mikopo.

Alisema hayo kwenye hafla ya kutoa mafunzo kwa wajasiriamali-350 wanawake kuhusu utumiaji mikopo kufanikisha uwekezaji. Alisema benki hiyo imejitolea kuwapa uwezo kina mama na vijana.

Takwimu kutoka benki ya IFC ambayo ni tawi la mikopo la benki kuu ya dunia zinaonesha kuwa asilimia-39 ya biashara zinaendeshwa na wanawake ilihaki ni chini ya asilimia-43 ya wanawake wanaopata mikopo.