Benjamin Netanyahu ashukiwa kuhushika katika uhalifu na ulaghai

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu anashukiwa kuhusika katika uhalifu unaohusisha utoaji wa hongo naA� ulaghai katika kesi mbili za ufisadi kwa mujibu wa polisi nchini humo. Katika kesi moja iliyopewa jina “File 1000,”, inadaiwa kuwaA� Netanyahu alipokea kwa njia isiyofaa zawadi kubwa kutoka kwa wafuasi wake matajiri akiwemoA� bilionare mmoja kutoka Australia James Packer na matayarishaji mmoja wa filamu wa Hollywood Arnon Milchan.A� Katika kesi ya pili kwa jina “File 2000,”, inadaiwa kuwa Netanyahu alijaribu kuafikia makubaliano na mchapishaji Arnon Mozes wa jarida laA� Yediot Ahronot ili kuchapisha sheria ya kudhoofisha mpinzani mkuu wa jarida hilo kwa minajili ya kutoa habari zinazompendelea Netanyahu. Netanyahu amekanusha madai hayo yote dhidi yake. Mawaziri wawili wakuu wa zamani wa IsraelA� Ehud Olmert na Ariel Sharon pia waliwahi kukabiliwa na madai ya ufisadi wakiwa afisini.