Bei ya petroli Aina ya Super yapungua Huku za Diseli na mafuta Taa Zaongezeka

Bei ya petroli aina ya super imepungua kwa  shilingi 4 na senti 87 kwa lita katika bei mpya za mafuta zilizotolewa na tume ya kuthibiti kawi .  Bei hizo mpya ziliaanza kutekelezwa kutoka saa sita za usiku  na kudumishwa hadi tarehe 14 mwezi mei mwaka huu.

Bei ya diseli imeongezeka kwa  senti 53 kwa  lita huku ile ya mafuta ya taa ikiongezeka kwa  shilingi 1 na senti 81. Kufuatia bei hizo mpya , bei ya petroli aina ya super sasa itakuwa shilingi  77 na senti 43 mjini Mombasa, shilingi 80 na senti 71 mjini  Nairobi, na shilingi  82 na senti 71 mjini Kisumu.

Diseli itauzwa  kwa shilingi 62 na senti 98 mjini Mombasa, shilingi 66 na senti  23 mjini  Nairobi na shilingi 68 na senti 40 mjini Kisumu. Mafuta ya taa yatauzwa  kwa  shilingi  41 na senti 27 mjini Mombasa, shilingi 43 na senti 96 mjini  Nairobi, na shilingi 45 na senti 86 mjini Kisumu.

Tume hiyo ilisema kuwa bei hizo mpya zinatokana na bei wastan ya kuagizwa kwa  petrol aina ya  super , dieseli na mafuta ya taa mtawalio katika miezi ya Februari na Machi .