Barnabas Korir awahimiza wakenya wawashabikie wanariadha wao nchini Australia

Kiongozi wa ujumbe wa Kenya utakaoelekea nchini Australia kushiriki michezo ya Jumuia ya madola, Barnabas Korir, amewahimiza wakenya wawashabikie wanariadha wa humu nchini katika michezo hiyo badala ya kuangazia makosa yaliyotekelezwa na ofisi ya kamati ya michezo ya Olimpiki iliyotangulia.

Kinara wa shirikisho la riadha, tawi la Nairobi, Barnabas Korir, atakayeuongoza ujumbe wa Kenya nchini Australia kushiriki kwenye michezo ya Jumuiya ya madola kuanzia tarehe 15 mwezi Aprili, amewaahidi wakenya kuwa mashindano hayo hayatakumbwa na utata wowote. Katibu mkuu wa NOCK F. K. Paul ameeleza kuwa kamati hiyo ina imani kuwa Korir ataongoza vyemaujumbewa Kenya. Wakati uo huo, baada ya kuandikisha matokeo duni jijini Rio, timu ya raga ya wanawake imeahidi kufanyaA� vyema nchini Australia.