Barcelona Yailaza Real Sociedad Na Kufuzu Nusu Fainali Ya Kombe La Copa Del Rey’

Aliyekuwa mchezaji wa Manchester City Denis Suarez aliifungia Barcelona mabao mawili na kuisaidia Barcelona kuandikisha ushindi wa mabao 5-2 na mabao 6-2 kwa ujumla dhidi yaA�A�Real Sociedad katika mchuano wa mkumbo wa pili kuwania kufuzu kwa nusu fainali ya mechi za kuwania ubingwa wa kombe la a�?Copa Del Reya��. Baada ya kushinda mechi ya mkumbo wa kwanza bao 1-0, Suarez aliongeza la pili kisha Lionel Messi akafunga la tatu kwa ujumla kupitia kwa mkwaju wa penalti. JuanmiA�A�aliifungia Sociedad dakika ya 62 kabla ya Luis Suarez kuifungia Barcelona bao la nne. Willian Jose’ aliifungia Sociedad la pili kabla ya Denis Suarez kufunga lake la pili na la tano kwa Barcelona liliipa ushindi wa mabao 5-2. Barcelona ambayo imeshinda taji hilo mara 28 sasa imefuzu kwa nusu fainali yake ya saba mtawalia.Timu nyingine ambazo tayari zimefuzu kwa nusu fainali ni mabingwa mara kumi waA�A�wa taji hilo la Copa Del Rey Atletico Madrid, Celta Vigo, naA�A�Alaves.Droo ya nusu fainali inatarajiwa kuandaliwa hii leo.