Baraza la usalama la umoja wa mataifa kupiga kura leo

Baraza la usalama la umoja wa mataifa linatarajiwa kupiga kura hivi leo, kuhusu rasimu ya azimio la umoja huo kuhusu hadhi ya mji wa Jerusalem, chini ya wiki mbili baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kuutangaza kuwa mji mkuu wa Israel. Hata hivyo, kuna uwezekano mkubwa kwa Marekani kutumia kura yake ya turufu katika kulipinga azimio hilo na kufanya lisiwe na maana yoyote. Baraza la usalama la umoja huo linajumuisha wanachama watano wa kudumu ambao ni:Marekani,Uingereza, China, Ufaransa na Russia, sawia na wanachama wengine 10 wasio wa kudumu. Kura ya turufu kutoka kwa yeyote kati ya wanachama wa kudumu itazuia kupitishwa kwa azimio hilo. Tangazo la Rais Trump lilichochea ghadhabu na maandamano ya Wa-Palestine na pia duniani kote, huku maandamano ya hivi punde na makubwa zaidi yaliandaliwa jana kwenye mji mkuu wa Indonesia, Jakarta, ambapo watu elfu-80 walikusanyika nnje ya Ubalozi wa Marekani mjini humo.Trump alitoa tangazo hilo tarehe 6 desemba, akisema siku hiyo kwamba Marekani itahamisha ubalozi wake kutoka Tel-Aviv hadi Jerusalem