Serikali na Baraza la magavana kutafuta suluhisho la mgomo wa wauguzi

Baraza la magavana na serikali ya kitaifaA� zimeitisha mkutano wa dharura ili kushughulikia mgomo unaoendelea wa wauguzi ambao sasa umeingia mwezi wa nne. Baraza hilo la magavana limesema kwamba iwapo juhudi za pamoja hazitafanywa, mgomo huo wa wauguzi utasambaratisha kabisa sekta ya afya nchini. Kulingana na mwenyekiti wa baraza hilo, gavana wa kaunty ya Turkana Josphat Nanok, mkutano huo uliliitishwa ili kujadilia ongezeko la migomo katika idara mbali mbali za sekta ya afya. Amesema mkutano huo wa ushauri utajadilia mzozo mkuu na kutafuta suluhisho la kudumu akiongeza kusema kwamba baadhi ya kaunty zinakumbwa na matatizo kwasababu ya mzigo mkubwa wa kuwalipa wafanyikazi wake mishahara na kwamba serikali za kaunty zimeshindwa kutekeleza matakwa ya wauguzi hao. Mawaziri wa fedha na afya, mwenyekiti wa tume ya kutathmini viwango vya mishahara na marupurupu ya watumishi wa umma na bodi ya utumishi wa uma wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo.A�