Baraza La Kitaifa La Mashirika Yasiyo Ya Serikali Yapongeza Uongozi Wa Jubilee Kwa Kukubali Kushiriki Katika Mashauriano Kutatua Mzozo Wa IEBC

Baraza la kitaifa la mashirika yasiyo ya serikali limempongeza rais Uhuru Kenyatta na uongozi wa Jubilee kwa kukubali kushiriki katika mashauriano ya kutatua mzozo kuhusu tume ya IEBC. Katika taarifa kwa wanahabari, baraza hilo lilisema hatua hiyo ni jambo la busara. Aidha taarifa hiyo ilisema mazungumzo kuhusu maswala yenye umuhimu wa kitaifa yanafaa na kwamba baraza hilo linatumai viongozi husika watatafuta suluhu kuhusu mzozo huo. Baraza hilo vile vile limehimiza kundi la viongozi kutoka bunge la seneti na lile la kitaifa kuunga mkono uamuzi wa rais na kujadili swala hilo kwa umakinifu.A�Baraza hilo pia lilihidi kuwasilisha maoni yake pale kamati husika itakapoanza kazi yao na kwamba litendelea kushiriki katika juhudi za kuhakikisha amani na maendeleo hapa nchini.A�Miungano ya CORD na Jubilee pia imeridhishwa na hatua hiyo ambayo itahakikisha amani na umoja miongoni mwa wakenya. A�