Barabara kadhaa Jijini Nairobi yafungwa kufuatia kuapishwa kwa rais

Polisi wamefunga barabara kadhaa Jijini Nairobi kwa matumizi ya umma kama mbinu mojawapo ya kiusalama kuhusiana na hafla ya leo ya kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto kwa muhula wa pili. Kamanda wa polisi katika Kaunti ya Nairobi, Japhet Koome, amesema kwamba barabara ya Mombasa kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, ile ya Uhuru Highway, Museum , Wangari Maathai, na pia barabara kuu ya Thika Superhighway hadi kwenye uwanja wa michezo wa Kasarani zitakuwa chini ya ulinzi mkali. A�Koome alitoa wito kwa waendeshaji magari sawia na watumiaji wengine wa barabara kuzingatia agizo jipya la Traffiki ili kurahisisha usafiri wa magari kuelekea kwenye uwanja wa michezo wa kimataifa wa Moi Kasarani, na pia eneo la kati-kati mwa Jiji.