Bao la Coutinho Yawamaliza Manchester United

Bao la kipekee lililofungwa na Philippe Coutinho lilididimiza matumaini ya Manchester United katika ligi ya Uropa huku Liverpool ikifuzu kwa robo fainali za kipute hicho baada ya kutoka sare bao moja kwa moja jana usiku uwanjani Old Traford.

Baada ya kufungwa mabao 2-0 katika mechi ya mkondo wa kwanza juma lililopita, United inayofunzwa naA� Louis van Gaal iliboresha matumaini ya kufuzu kwa mechi za mchujo wakatiA� Anthony Martial alipofunga bao lake la 32A� uwanjaniA� Old Trafford.

Lakini bao lililofungwa na Coutinho muda mfupi kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika lilididimiza matumaini ya Manchester United ya kufuzuA� huku Liverpool ikifuzu kwa jumla ya mabao 3-1.

Katika mechi nyingine zilizochezwa jana usiku,Valencia iliinyuka Athletic Bilbao mabao mawili kwa moja huku Tottenham ikilazwa mabao mawili kwa moja na Borussia Dortmund. Sevilla iliipiku Basel mabao matatu kwa sifuri huku Bayern Leverkusen ikitoka sare kappa na Villareal.