Benki Kuu Ya Kenya Yatia Benki Ya Chase Chini Ya Mrasibu Kwa Muda Wa Miezi 12

Benki ya Chase imewekwa chini ya mrasibu kwa muda wa miezi 12 kufuatia kile Benki Kuu ya Kenya ilichotaja kuwa wasiwasi wa kifedha kwenye benki hiyo. Gavana wa Benki kuu ya Kenya Dr. Patrick Njoroge alisema benki hiyo inakumbwa na changamoto za kifedha. Hatua ya Benki kuu ya Kenya ya kuiweka benki ya Chase chini ya mdhamana hata hivyo haikutarajiwa na wateja wake. Ishara kwamba kulikuwa na hali ya mshikemshike kwenye benki ya Chase zilichipuza hapo jana wakati mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo Zafrullah Khan na mkurugenzi mkuu Duncan Kabui walipojiuzulu.