Balvo kuchukua nafasi ya marehemu Cornelius Korir

Kanisa katoliki litamteua kaimu askofu atakayechukua mahala pa marehemu askofu Cornelius Korir aliyezikwa siku ya Jumamosi. Kuligana na mwakilishi wa baba mtakatifu Francis hapa nchini askofu Charles Daniel Balvo, huenda ikachukua muda kumpata atakayechukua mahala pa askofu Korir. Askofu Balvo alitangaza hayo wakati wa hafla ya mazishi ya marehemu askofu Korir iliyoandaliwa katika uwanja wa michezo wa Eldoret. Viongozi hata hivyo wamelihimiza kanisa katoliki kumtafuta atakayeendeleza kazi ya marehemu askofu Korir. Mwili wa marehemu askofu Kori ulizikwa katika kanisa la Sacred Heart Cathedral mjini Eldoret. Kulingana na kanuni za dini ya kikatoliki askofu anayeaga dunia akiwa yungali mamlakani anaweza kuzikwa ndani ya kanisa A�au katika mahala maalum panapotayarishwa na maaskofu.