Balala Ahimiza Uingereza Kuondoa Tahadhari Ya Usafiri Lamu

Waziri wa utalii Najib Balala amehimizaA�Uingereza kuondoa tahadhari ya usafiri iliyotangazwa katika kaunti ya Lamu ili kuimarisha sekta ya utalii katika eneo hilo. Uingereza ilitangaza tahadhari hiyo ya usafiri katika kisiwa cha Lamu na viunga vyake kwa muda wa miaka mitano iliyopita tangu kutekwa nyara kwa watalii wawili raia wa Ufaransa na Uingereza mnamo mwaka 2011. Akiongea huko Lamu wakati wa warsha ya wadau katika sekta ya utalii, Balala alitoa wito kwa balozi wa Uingereza hapa nchini Nic Hailey kuiarifuA�serikali ya Uingereza kuwa i ya usalama umeimarishwa hapa nchini kufuatia operesheni ya Linda nchi katika eneo hilo. Matamshi ya Balala, yalitiliwa mkazo na gavana wa Lamu Issa Timamy aliyesema kuondolewa kwa tahadhari hiyo ya usafiri kutaimarisha mapato ya kaunti hiyo na biashara nyingine ambazo zimedidimia kutokana na ukosefu wa watalii. Hata hivyo serikali ya uingereza haionekeni kukukabiliana na maoni hayo. Balozi huyo alisema kutokana na makadirio ya kila wiki ya serikali ya Uingereza ,hali ya usalama bado hairidhishi katika eneo hilo kuwezesha kuondolewa kwa tahadhari hiyo.