Babu Owino aachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki mbili

Mbunge wa Embakasi MasharikiA� Paul Ongili almaarufu Babu Owino jana aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki mbili baada ya kukanusha mashtaka ya kudhuru na kutumia nguvu nyingi kupita kiasi wakati wa uchaguzi mkuu wa tarehe nane mwezi Agosti mwaka huu.A� Owino alifika mbele ya hakimu mkuuA� Joyce Gandani katika mahakama ya Kibera baada ya kulala korokoroni kwa siku tatu. Alikanusha mashtaka ya kumdhuru Joshua Otieno Obiende wakati wa uchaguzi mkuu uliopita. Akitangaza dhamana hiyo, Gandani alisema kuwa upande wa mashtakaA� haukutoa ushahidi wowote wa kuonyesha kuwa mshtakiwa angevuruga ushahidi na hivyoA� kumnyima dhamana kungesababisha ghasia. Hata hivyo hakimu huyo alimuonya Babu Owino kuwa mahakamaA� haitasita kufutilia mbali dhamana hiyo iwapo atafanya makosa sawa na hayo. Kesi hiyo itasikizwa tarehe 5 mwezi Disemba mwaka huu.