Babu Owino akumbwa na pigo baada ya mahakama kuu kuagiza kuhesabiwa upya kwa kura za eneo lake

Mbunge wa Embakasi mashariki, Babu Owino, amekumbwa na pigo baada ya mahakama kuu kuagiza kuchunguzwa na kuhesabiwa upya kura za eneo bunge la Embakasi mashariki kuhusiana na uchaguzi mkuu wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka uliopita. Kwenye uamuzi wake, jaji Joseph Sergon aliamua kwamba mwasilishi wa rufaa hiyo Francis Mureithi alitoa sababu za kutosha za kuhesabiwa tena kwa kura hizo. Mureithi ambaye anapinga kuchaguliwa kwa Babu Owino kuwa mbunge wa Embakasi mashariki alikuwa amewasilisha rufaa ya kutaka kuchunguzwa na kuhesabiwa upya kura zilizopigwa wakati wa uchaguzi mkuu mwezi Agosti mwaka jana. Jaji Sergon kwenye uamuzi wake alisema kwamba afisa aliyesimamia uchaguzi katika eneo bunge la Embakasi mashariki alikiri mahakamani kwamba matokeo alioyatangazaA�A�hayakuwiana na yale yaliokuwa kwenye fomu za 35 A. Kwingineko,A�seneta wa wa MeruA�Mithika Linturi amepinga ombi la kutaka kesi ya kupinga ushindi wake iondolewe mahakamani.Kupitia kwa wakili wake Prof Tom Ojienda,seneta huyo wa Meru anataka mahakama itupilie mbali ombi hilo laA�Mugambi ImanyaraA�A�kwasababu linakiuka taratibu za kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi. Jaji Ann Ongijo ataamua kesi hiyo tarehe 20 mwezi huu.