Babu Owino akamatwa tena pindi tu baada ya kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu 500

Mbunge wa eneo la Embakasi masharikiA� Paul Ongili almaarufuA� Babu Owino jana alikamatwa tena pindi tu baada ya kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi nusu milioni kuhusiana na madai ya jumbe ambazo amekuwa akituma katika mtandao wa kijamii wa twitter. Owino alilala korokoroni kwa siku ya pili Jumanne baada ya upande wa mashtaka kupinga ombi lake la kutaka kuachiliwa kwa dhamana.A� Siku ya jumatano alifika mbele ya hakimu mkuu Francis Andayi katika mahakama yaA� Milimani jijiniA� Nairobi ambapo alikanusha mashtaka matatu dhidi yake. Huku akimtambua Owino kuwa mbunge,A� Andayi alisisitiza kuwaA� jumbe za chuki zinazosambazwa katika mitandao ya jamii na katika mikutano ya kisiasa nchini ni hatari kwa udhabiti wa taifa hili. Upande wa mashtaka ulikuwa umepinga kuachiliwa kwake kwa dhamana ukisema kuwa kosa hilo lilistahili adhabu kali na lakini upande wa utetezi ukafutilia mbali pingamizi hiyo. A�