Baadhi ya wabunge wasifu hotuba ya Uhuru iliyogusia maswala yanayowaathiri wakenya

Baadhi ya wabunge wamesifu hotuba ya rais Uhuru Kenyatta kwa taifa ambayo wamesema iligusia maswala yote yanayoathiri wakenya. WabungeA�A�Chachu Ganya wa Hor Kaskazini , Janet Nangabo wa Trans Nzoia na Zachayo Cheruiyot wa Kuresoi Kusini wamesema serikali yaA�A�Jubilee imeunga mkono kikamilifu mfumo wa ugatuzi kuambatana na katiba. Wamesema serikali yaA�A�Jubilee imekuwa katika mstari wa mbele katika kukidhia ustawi katika viwango vya magatuzi kwa kutoa ruzuku. Wabunge walisema hayo walipokuwa wakijadili hotuba ya rais kwa taifa iliyotolewa siku ya Jumatano wiki iliyopita.A�A�Akiunga mkono kupelekwa kwa maafisa wa KDF nchini Somalia Nangabo alisema mipaka ya nchi hii sasa ni salama huku Somalia ikiwa na udhabiti. Wakati huo huo Nangabo alisema nchi hii ingali inakumbwa na jinamizi la ufisadi. Wakichangia mjadala huo wabunge wa upinzaniA�A�Michael Onyura wa Butula, Yusuf Chanzu wa Vihiga, Patrick Makau wa Mavoko na Abdikadir Ore wa Wajir Magharibi walisema hotuba ya rais ilikosa kuwapa wakenya matumaini.Walitaja viwango vya juu vya ukosefu wa ajira miongoniA�A�mwa vijana .A�A�Walisema licha ya serikali ya Jubilee kuahidi kubuni nafasi za ajira kwenye manifesto yake wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2013 kampuni nyingi zimeamua kuhamia nchi nyingine barani Afrika ikiwemo Zambia.