Baadhi Ya Viongozi Wa Jubilee Waeleza Kuunga Mkono Chama Ambacho Hakijazinduliwa Cha Jubilee

Baadhi ya viongozi wa Jubilee wameeleza kuunga mkono chama ambacho hakijazinduliwa cha Jubilee wakisema Wakenya sharti wakiunge mkono chama hicho kwa minajili ya umoja. Wakiongea huko Chesewew, Marakwet wakati wa mkutano wa kuchanga pesa, viongozi hao Kipchumba Murkomen, mbunge wa Cheseret Oscar Sudi ba gavana Alex Tolgos, walisema chama cha Jubilee kitaanda uteuzi wake kupitia kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka-IEBC ili kukabilianaA�A�na hali ya kuto-ridhika katika chama hicho kipya cha kisiasa. Murkomen alisema hatua hii itahakikisha wanachama wana umoja na hivyo kuthibiti hali ya kuvihamia vyama vingine. Chama cha Jubilee kitazinduliwa mwezi Septemba lakini ni chama cha Ford-Kenya pekee ambacho kimevunjiliwa mbali na kujiunga na chama hicho. Gavana wa Meru, Peter Munya, ametangaza kwamba atatetea kiti chake kwa tiketi ya chama cha PNU mwaka ujao ilhali mwenzake wa Bomet Isaac Rutto atawania kuchaguliwa tena kwa tikiti ya chama cha Mashinani. Chama cha Kanu pia kimetangaza kwamba hakitavunjiliwa mbali ili kujiunga na chama cha Jubilee.