Baadhi Ya Mashirika Ya Kijamii Yaishauri Serikali Kutofunga Shule Kufuatia Msururu Wa Visa Vya Uharibifu Shuleni

Baadhi ya mashirika ya kijamii yameishauri serikali kutofunga shule kufuatia msururu wa visa vya uharibifu wa mali shuleni. Akiongea baada ya kukutana na waziri wa elimu, Fred Matianga��i mashirika hayo badala yake yaliwahimiza wazazi kuunga mkono juhudi za serikali za kufanyia marekebisho sekta ya elimu. Aidha walitoa wito kwa wizara ya elimu kutokubali wito wa chama cha walimu wa kufunga shule zote ili kuepusha uharibifu zaidi wa mali ya shule. Wakiongozwa na Janet Ouko wa shirika la Elimu yetu, mashirika hayo ya kijamii pia yaliwashauri walimu wakuu wa shule kuhakikisha kwamba wanawashirikisha wazazi na wanafunzi katika kubuni sheria au miradi mipya.

Waziri wa elimu, Fred Matianga��i alikutana faraghani na mashirika ya kijamii kujadilia swala la migomo ya shule.