Ayiecho Olweny apoteza kesi ya kupinga uteuzi wa Ka��Oyoo

Mahakama ya juu imetupilia mbali kesi inayopinga uteuzi wa James Onyango Ka��Oyoo kuwa mgombea uchaguzi wa chama cha ODM katika eneo bunge la Muhoroni. Kesi hiyo iliwasilishwa na Profesa Ayiecho Olweny. Kesi hiyo ilisikizwa jana na jaji mkuu David Maraga, naibu jaji mkuu Philomena Mwilu na majaji ya mahakama ya juu Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala na Isaac Lenaola wakati wa kikao maalum cha mahakama ya juu. Profesa Olweny alisema kwamba Ka��Oyoo, ambaye alitangazwa mshindi wakati wa uteuzi wa chama cha ODM na kukabidhiwa cheti aliteuliwa kikamosa na chama hicho.