Atwoli amtaka Raila akome kutoa vitisho kuhusu uchaguzi ujao

Katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyikazi a��COTU, Francis Atwoli, amemtaka kiongozi wa muungano wa NASA, Raila Odinga kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi wa Urais tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu na akome kutoa vitisho kwamba hakutakuwa na uchaguzi. Akiongea katika eneo bunge la Khwisero, kaunti ya Kakamega, katibu mkuu huyo wa COTU kadhalika alimtaka pia waziri mkuu huyo wa zamani, kufanya kampeni kote nchini kabla ya kinyanga��anyiro baina yake na Rais Uhuru Kenyatta.Atwoli alimtaka Raila kuendeleza kampeni kote nchini na akome kulalama kwamba hakushauriwa kuhusu tarehe ya marudio ya uchaguzi na tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC.

Wakati huo huo, Atwoli alimtaka Rais Kenyatta kuheshimu uhuru wa idara wa mahakama.