Atwoli ahimiza mirengo ya Jubilee na NASA kuyakubali marekebisho ya IEBC

Katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini-(COTU), Francis Atwoli, amehimiza viongozi wa mirengo ya JubileeA� na NASA, kuyakubali marekebisho fulani A�yanayotekelezwa na tume ya -IEBC , kabla ya marudio ya uchaguzi wa Urais mnamo tarehe 17 Octoba mwaka huu. Kwenye taarifa kwa vyumba vya habari, Atwoli aliwataka viongozi wote kufahamu kwamba nchi hii inazidi kuathirika kiuchumi, na kwamba Wakenya hawafai kuwekwa katika hali ya heka heka na malumbano ya kisiasa nyakati zote. Atwoli A�alisema kwamba mizozo inayoendelea, imewaogofya wawekezaji na jamii ya wafanyibiashara kwa ujumla A�hali ambayo huenda ikasababisha kupotea kwa nafasi za kazi. Alisema kwamba viongozi wa kisiasa wanapaswa kuikubali terehe ya marudio ya uchaguzi wa Urais iliyopendekezwa IEBC, ikizingatiwa kwamba mahakama iliwapa muda wa siku 60, na zimebakia siku 39 pekee hadi sasa. Alisema kwamba muungano wa COTU unatumai kwamba wanasiasa wa mirengo yote wataafikiana na tume ya IEBC, na kusuluhisha kwa amani tofauti zilizoko ili kufungua milango kwa uchaguzi wa amani. Wakati huo huo; Atwoli amehimiza wakenya kuyakubali matokeo ya marudio ya uchaguzi huo wa Urais, na kudumisha amani huku taifa hili likijaribu kujikwamua kiuchumi.