Atwoli afurahia uteuzi wa baraza la mawaziri

Katibu mkuu wa muungano wa wafanyikazi nchini, COTU, Francis Atwoli amepongeza uteuzi wa hivi maajuzi wa baraza la mawaziri huku akisema kuwa hali hiyo itasaidia kusukuma ajendaA� ya serikali kuhusu maendeleo. Atwoli ambaye alikuwa akiongea jana katika makao makuu ya COTU jijini Nairobi, alifurahia kupendekezwa kwa aliyekuwa seneta wa kaunti ya TurkanaA�A�John Munyes, huku akitoa wito wa kuteuliwa kwake kuwa waziri wa leba na huduma za jamii kwa vile ana ufahamu mwema wa maswala ya leba hasa baada ya kuhudumu katika wadhifa huo hapo kabla.

Atwoli alimpongeza rais kwa kumhifadhi Fred Matianga��I katika baraza la mawaziri na lakini akasema kuwa angehifadhiwa katika wizara ya elimu ambapo alikuwa ameanzisha marekebisho maalum badala ya kuwekwa katika wizara ya usalama wa kitaifa