Atwoli aandaa mkutano kuunganisha jamii ya Waluhya

 

Katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyakazi hapa nchini COTU Francis Atwoli ameandaa mkutano nyumbani kwake huko Khwisero kaunti ya Kakamega kwa lengo la kuimarisha umoja wa jamii ya Waluhya . Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi na viongozi kadhaa wa jamii ya Waluhya. Duru zinaashiria kuwa lengo kuu la mkutano huo ni kupanga mikakati ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022. Aliyekuwa mwanasheria mkuu aliye pia seneta wa kaunti ya Busia A�Amos Wako na mbunge wa A�Emuhaya Omboko Milemba ni miongoni mwa viongozi wengine kutoka jamii hiyo waliohudhuria mkutano huo. Mkutano huo umejiri baada ya matamshi ya hivi majuzi ya Atwoli kuwa anajutia kupaanga karamu ya kumteuwa Musalia Mudavadi kuwa msemaji wa jamii ya Waluhya . Alitoa matamshi hayo baada ya A�Mudavadi pamoja na seneta wa A�Bungoma Moses Wetangula na Kalonzo Musyoka kukosa kuhudhuria hafla ya kumwapisha A�Raila Odinga kuwa rais wa watu