Assange Adai Atajisalimisha Kama U.N Itakanusha Mashtaka Dhidi Yake

Mwasisi wa mtandao wa Wikileaks, Julian Assange amesema atajisalimisha kwa mafisa wa polisi wa Uingereza hapo kesho iwapo jopo la Uingereza litaamua kwamba hajazuiliwa kinyume cha sheria. Alitafuta uhifadhi katika ubalozi wa Uingereza nchini Ecuador mwaka-2012 ili kuepuka kurejeshwa nchini Sweden kujibu mashtaka ya dhuluma za kimapenzi. Mnamo mwaka-2014 alilalamikia Umoja wa Mataifa kwamba alikuwa akizuiliwa kiholela kwani hangeondoka bila kukamatwa. Polisi wa kimataifa wanasema Assange, ambaye anakanusha madai dhidi yake, atakamatwa pindi atakapoondoka kwenye ubalozi huo. Ofisi ya mashauri ya kigeni ya Uingereza ilisema Assange alikuwa ameepuka kimaksudi kuzuiliwa kihalali, ikisema ingali ina jukumu la kumrejesha nchini Sweden. Hayo yanajiri huku jopo la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia suala la kuzuiliwa kiholela likitarajiwa kutangaza matokeo ya uchunguzi wake kuhusu kisa cha Assange hapo kesho. Assange alikamatwa mjini London mwaka-2010 chini ya kibali kilichotolewa na Sweden. Shirika lake la mtandao wa Wikileaks lilisakini hati za siri za serikali ya Marekani kwa mtandao na Assange anasema anaamini Marekani itataka apelekwe nchini humo iwapo atarejeshwa nchini Sweden.