Asilimia 53 Ya Wakenya Wasema Nchi Haifuati Mkondo Unaofaa-Info track

Matokeo ya kura ya maoni yaliyotolewa na kampuni yaA� info track yanaonyesha kuwa asilimiaA� 53 ya wakenya wanahisi nchi haifuati mkondo unaofaa.A� Hata hivyo idadi hiyo imepungua kwa asilimia 9 ikilinganishwa na mwezi Oktoba mwaka uliopita ambapo idadi hiyo ilikuwa asilimia 62. Kwenye utafiti huo ,ufisadi, ukosefu wa ajira na gharama ya juu ya maisha ndiyo yanayowakera wakenya wengi.Kulingana na afisa mkuu wa kampuni hiyo Angela Ambitho wasiwasi miongoni mwa Wakenya umepungua kiasi kufwatia kupungua kwa visa vya mashambulizi ya kigaidi mwaka huu ikilinganishwa na mwaka uliopitaA� pamoja na kujitolea kwa rais katika kupambana na ufisadi.