Asenali yatumai kumaliza katika nne bora

Mlinzi wa Asenali, Shkodran Mustafi, amesema kuwa anatumaini timu hiyoA� imesitisha msururu wa matokeo duni ili kumaliza katika nafasi nne bora katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Asenali iliishinda Southampton mabao mawili kwa bila siku ya Jumatano, huku ikichupa hadi nafasi ya tano, alama tatu nyuma ya Manchester City na kusalia na mechi tatu msimu utamatike. Mkufunzi, Arsene Wenger, hajawahi kukosa kumaliza katika nafasi nne bora ligini tangu aanze kukifunza kilabu hicho, chenye makao yake Kaskazini mwa jiji la London, na ana uhakika timu hiyo itafuzu kwa ligi ya mabingwa kwa mara nyingine, licha ya kupoteza mechi 6 kati ya 11 ligini. Hata hivyo, Asenali itanuia kuboresha matumaini yake ya kufuzu kwa ligi hiyo itakapochuana na Stoke City, kesho na kuboresha uwezekana wa kufuzu kwa ligi ya mabingwa Barani Ulaya.