Asenali yanuia kutamatisha msururu wa matokeo duni

Asenali inanuia kutamatisha msururu wa matokeo duni itakapochuana na AC Milan, katika mechi ya mkondo wa kwanza, raundi ya 16 bora ya ligi ya Bara Ulaya leo usiku uwanjani San Siro.

Timu hiyo inayofunzwa na Arsene Wenger, imeshindwa mechi nne mfululizo, hii ikiwa mara ya kwanza kuandikisha matokeo hayo tangu mwezi Oktoba mwaka 2002.A� Asenali itazikosa huduma za Hector Bellerin, Nacho Monreal na Alexandre Lacazette waliojeruhiwa sawa na Pierre-Emerick Aubameyang.A� AC Milan, chini ya ukufunzi wa Gennaro GattAuso, haijashindwa katika mechi 13. Aidha, timu hiyo inashikilia nafasi ya saba katika ligi kuu ya soka nchini Italia kwa alama 44, alama 25 nyuma ya vinara Napoli, lakini iliishinda Lazio na kufuzu kwa fainali ya a�?Coppa Italiaa�� na haijafungwa bao hata moja katika mechi sita za mwisho ilizocheza. Jumla ya mechi nane za ligi hiyo ya Bara Ulaya zitachezwa leo usiku.